Sunday, June 10, 2012


STARS YAWASHA INDIKETA SAFARI YA BRAZIL 2014

Kikosi kilichofanya mauaji leo
 Erasto Nyoni mfungaji wa bao la ushindi
Shomary Kapombe aliyesawazisha
 Boban akisaidia ulinzi
 Boban kabla ya kuingia kulia akiwa na Nurdin Bakari benchi
 Boban kulia, Nurdin katikati na Shaabn Nditi

 Dk Mwankemwa akimtibu jeraha Ngassa
Kaseja akiokoa moja ya hatari langoni Stars
Mwinyi Kazimoto akiwaongoza wenzake kutoka uwanjani baada ya mechi

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya pili ya Kundi C, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Stars ilitoka nyuma kwa 1-0 kipindi cha kwanza na kuibuka na ushindi huo- kwa mabao ya kipindi cha pili ya Shomari Kapombe dakika ya 60 na Erasto Nyoni dakika ya 87 kwa penalti, baada ya beki mmoja wa Gambia kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Stars ambayo mechi ya kwanza ilifungwa 2-0 na wenyeji Ivory Coast mjini Abidjan Jumamosi iliyopita, kipindi cha kwanza ilicheza ovyo kidogo, lakini kuingia kwa Haruna Moshi ‘Boban’ aliyechukua nafasi John Bocco ‘Adebayor’ kipindi cha pili, kuliifanya Tanzania icheze kwa uhai na kulitia misukosuko lango la Gambia hatimaye kupata mabao hayo mawili.
Gambia walitangulia kupata bao lililofungwa na Mamadou Ceesay dakika ya nne.
Stars sasa imejinasua mkiani mwa kundi C na kupanda nafasi ya pili badaaye Morocco kutoa sare ya 2-2 jana na Ivory Coast inayoongoza kwa pointi zake nne.
Kwa Stars huu ni ushindi wa kwanza nyumbani tangu waifunge Jamhuri ya Afrika ya Kati Machi 26, mwaka jana.


Vikosi vya Tanzania kushoto na Gambia kulia

Mfungaji wa bao la Gambia dakika ya nane, Mamadou Cesay akishangilia

No comments:

Post a Comment