Timu ya Tanzania Houston Community jana katika viwanja vya Cullen Park, Houston Texas walifanikiwa kuichapa Tanzania New York Community kwa mabao 5–1 katika mchezo maalum wa kusherehekea Uhuru wa Marekani.
Mechi hiyo ilihudhuriwa na Watanzania waishio Houston na miji ya karibu ilikuwa ya ushindani mkubwa. Vijana wa Houston walijipatia magoli yao kupitia kwa Ali Ngolo dk 16, Said Mvano dk 29, Claude Mukeha dk 54, Heri Jr dk 76 na Dalva Furaha dk ya 89. New York walijipatia bao la kufutia machozi kupiti kwa mshambiliaji wao msumbufu Hussein dk ya 69 ya mchezo.
Ilikuwa mechi ya ushindani, ushindani wa kiutamaduni na umoja, lakini vijana wa Houston walionyesha ubora, nidhamu na kasi tangu dakika za mwanzo. Ushindi huu si tu matokeo ya uwanjani, bali ni ishara ya nguvu, umoja na moyo wa Watanzania wanaoishi Houston.
Hongera sana Tanzania Houston Community! Ushindi wa 5–1 ni fahari ya jumuiya na motisha ya kuendelea kuimarisha michezo na umoja wetu.
Pata picha za tukio hilo;


.jpg)
.jpg)


