Friday, August 10, 2012

Hali ya uuzaji wa madawa ya binadamu kiholela jijini Dar es Salaam inatisha



 Matokeo haya yametokana na utafuti ulifanywa na YITA Novemba 2011 na ulihusisha watafitit waliofanya ziara siri (mystery shoppers) 126 katika maduka 64 ya wilaya zote tatu za Dar es salaam. Jina la muhtasari wenye matokeo hayo ni “Ununuzi wa dawa jijini Dar es Salaam-Je, maduka ya dawa yanazingatia kanuni?” . Pamoja na mengine watafiti waliweza kuhoji yafuatayo;

Je, dawa zinaweza kutufanya wagonjwa? Je, zinatolewa ipasavyo? Na je, mfumo wa kuwalinda wananchi kutokana na madhara ya matumizi mabaya ya dawa unafanya kazi vizuri?


Ikumbukwe mamlaka ya dawa na chakula Tanzania imetamka wazi kwenye  Kifungu cha 31:3 ya viwango vya biashara ya dawa nchini ya mwaka 2006 (Pharmaceutical Business Standards Regulations) kuwa;
“Hakuna mtoaji dawa yeyote atakayetoa dawa ambazo matumizi yake yanapaswa kuwa kwa maagizo ya daktari tu isipokuwa kwa agizo la matumizi ya dawa husika lililotolewa na mfanyakazi wa afya, mganga wa meno au wa mifugo au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa kuagiza matumizi ya dawa”.


Utaafiti imedhihirisha ukiukwaji mkubwa wa kanuni za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).Ni wazi madhara yafuatayo yataliandama Taifa kama hatua za dhati hazitachukuliwa haraka;

Uwezekano wa wagonjwa kutumia dawa katika vipimo visivyo sahihi ambavyo vinaweza kusababisha dawa kushindwa kutibu tatizo lao na kusababisha pia matatizo mengine, ikiwa ni pamoja na dawa kuwa sumu mwilini
Wagonjwa wanaweza kuishia kutumia dawa zisizo sahihi kwa matatizo ya kiafya waliyo nayo na hivyo kuziweka afya zao hatarini
Wagonjwa wanaweza kujenga utegemezi kwa dawa fulani.

Mbali na kwamba utafiti huu haukufuatilia kwa kina sababu zinazopelekea tatizo hili kukithiri hisia za wengi zinahoji haya;

Je, inawezekana kwamba wahudumu katika maduka ya dawa hawajapata mafunzo ya kutosha na hawana uelewa?

Je, wana uelewa lakini msukumo toka kwa wamiliki kupata faida, ukichanganywa na mfumo hafifu wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa kanuni vinawafanya wapuuze maarifa waliyonayo na kuuza dawa bila kuzingatia kanuni?

Je, msukumo mkubwa wa hali hii unatokana na matarajio ya wananchi wenyewe ya kupata dawa kwa haraka na urahisi, bila gharama kubwa, bila shida na wakati mwingine bila unyanyasaji wanaofanyiwa wakiwa mikononi mwa wahudumu wa afya?

Iwapo tunajali kuhusu afya na hali bora za watu, kushughulikiwa kwa maswali haya na kutafuta ufumbuzi unaofaa ni jambo la msingi linalopaswa kufanywa na TFDA, Wizara ya Afya na wananchi kadhalika. Pia kuhakikisha kanuni zilizowekwa zinafatiliwa na kusimamiwa kwa manufaa na ustawi wa wananchi na uhai wa Taifa.

No comments:

Post a Comment