Monday, November 26, 2012

KAMANDA WA POLISI ATHIBITISHA KIFO CHA HUSSEIN "SHARO MILLIONEA " MKIETY


Msanii  Hussein Ramadhani aliyekuwa maarufu kwa jina la Sharo Millionea, msanii wa muziki na maarufu katika kuwepo kwake katika matangazo kwa style ya aina yake amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari Tanga. 


 Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constatine Masawe amekiri kutokea kwa msiba wa Sharobaro, baada ya kupata ajali katika kijiji cha Lusanga, Muheza ambapo pia ndio nyumbani kwao






 Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”


Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.


R.I.P SHARO MILLIONEA 

No comments:

Post a Comment