Sunday, December 2, 2012

Houston African Cup Semi Final : Tanzania 0-1 Liberia

Kikosi cha Tanzania kilichoanza leo
Timu ya soka ya Watanzania waishio Houston Texas jioni ya leo ilitolewa kwa taabu na Liberia kwenye nusu fainali ya michuno ya Africa.Ikicheza kandanda safi Tanzania ilimiliki kwa kiasi kikubwa mchezo huo lakini bahati haikuwa upande wao siku ya leo.

Tanzania ilipata penati baada ya beki wa Liberia Pape Sarr kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari katika dakika ya 82. Raheem Toure alipiga penati hiyo kiufundi lakini ikatoka mita chache pembeni mwa lango la Liberia.

Bao la ushindi la Liberia lilifungwa na mshambuliaji  James Debbah dakika ya 85 ya mchezo baada kipa wa Tanzania John Kijani kutema shuti la mpira wa adhabu.

Timu ya Tanzania ilikuwa bora katika michuano hii hasa ikizingatiwa timu ya mwisho ya Tanzania kufika fainali ya michuano hiyo ilikuwa ni ya mwaka 2002 na kufungwa 1-0 na Nigeria.Vijana walitaka kuvunja rekodi hiyo mwaka huu lakini bahati haikuwa upande wao.

Sekulu akimkimbiza beki Fahnibuller wa Liberia
Justice akitoa pasi kwa Muddy Chamshama ambayo ilipelekea beki wa Liberia kuunawa na kutoa penati

Beki Pape Sarr akiunawa mpira

Raheem Toure akikosa penati dakika ya 82

Wadau baada ya mechi

Wadau baada ya mechi

Wadau baada ya mechi

Wadau baada ya mechi

No comments:

Post a Comment