Friday, January 18, 2013

Simba SC yalala tena Umangani 3-1

MABIGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom, Simba SC wameendelea kufanya vibaya katika michezo yao ya kirafiki nchini Oman baada ya leo kutandikwa mabao 3-1 na timu ya ya Qaboos,katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Qaboos nchini Oman.
Kwa mujibu kocha wa zamani wa Simba mwenye makazi yake nchini Oman, Talib Hilal alisema licha ya kipigo hicho, Simba ilionesha kandanda safi na ya kuvutia, huku bao la kufutia machzi la Simba lilipachikwa na mshambuliaji, Haruna Moshi ‘Boban’.
Simba ambayo ipo huko tangu wiki iliyopita, kwa kambi maalum ya kujiandaa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika, juzi ilitandikwa bao 1-0 na timu ya taifa ya soka ya Oman chini ya umri wa miaka 23.
Aidha, Simba inayonolewa na Patrick Liewig inatarajiwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki na Fanja Fc, kabla ya kurejea nchini Januari 23 tayari kwa kuanza mzunguko wa pili wa Ligi unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 26.

No comments:

Post a Comment