Kwa muda mrefu nimekuwa nikitoa
hamasa kwa vijana wenzangu wa kike na kiume na watu wa kada mbalimbali, wito
wangu umekuwa nikuwataka vijana wenzangu kauanza utamaduni wa kuwekeza kwa muda
mrefu na kujifunza ujasiriamali.
Nilipoandika makala Yenye kichwa
cha KWENYE UJASIRIAMALI NG’OMBE WA
MASIKINI HUZAA,nilisema kwamba, ‘Ukifikiri
kuhusu maisha ya hapa duniani hasa kwa kuangalia mfumo wa maisha kwa kila
binadamu tukianzia kwa walemavu,ombaomba,maskini,wagonjwa,vichaa,wanaohangaika
usiku na mchana kwaajili ya chakula tu na nguo za kuficha utupu wao na makundi
mengine lazima utafika mbali sana na kufika mahali na kukubali kuwa kuna kitu
hakijakamilika katika maisha ya hapa duniani.
Au unaweza kuhisi kana kwamba
dunia hii ina mapungufu sana.Najua kwa mwingine anaweza
kusema hayo yote ni mipango ya Mungu na kuishia hapo’.
Ukifikifiri tena kuhusu matajiri wa dunia hii akina Reginald Mengi, Yusuf Manji, Bill Gates, Carlos Slim,marehemu Steve Jobs, Warren Buffet, Bernard Arnault na Larry Ellison lazima utajikuta kuwa kuna shida kuelewa hiyo mipango au majaliwa ambayo wengi huamini kuwa ni ya Mungu kwa watu hawa huwa kama walivyo. Hebu turudi katika uhalisia wa maisha.
Ninaandika makala hii, kutoa ushuhuda wa niliyoyafanya kwa muda wa miaka miwili iliyopita,na pia ninaandika makala hii kujibu baadhi ya maswali ambayo baadhi ya rafiki zangu wamekuwa wakiniuliza. Nilianza kujishighulisha na ujasiriamali nilipokuwa chuo kikuu mwaka wa pili, kwa kuuza vocha na kazi ya ‘steshenari’ na uuzaji wa laptop, sikuendelea nazo sana kwa sababu ya kubanwa na masomo ya chuo. Nilipomaliza chuo 2010, nilianza kilimo cha mboga na kufuga kuku hapa Iringa mjini,baada ya hapo kaka yangu alianza kunihimiza kuhusu kilimo cha miti ambacho yeye mwenyewe anafanya. Na baadae nikakutana na rafiki yangu Albert Sanga ambae anafanya pia kilimo cha miti kwa sana.
Tangu 2011 nilinunua shamba la ekari 10 na kuzipanda miti hela ambayo niliipata baada ya kuuza matango niliyolima kijijini Kalenga,nikaongeza bidii zaidi ya kulima matango na kununua mashamba,leo nina ekari nyingi.
Albert Sanga, mjasirimali na
mwekezaji alipata kuandika haya kuhusu mimi:-“UNASUBIRI
UPATE MTAJI? OPSIII! UNAWEZA KUFA MASIKINI!
Nina rafiki yangu mpambanaji kweli kweli na msomi wa
chuo kikuu wa mambo ya maendeleo na elimu; na mtaalamu wa IT, anaitwa Meshack Maganga. Wakati fulani huko nyuma alinifuata na kuniambia,
"Sanga nimeamua kuanza kui-invest katika mashamba ya miti; mtaji wa
kuanzia nina tsh elfu ishirini na tano, (25,000?/=). Nikamwambia "Kupata
ekari moja si chini ya laki sita na wewe una
tsh 25,000/= utawezaje?" Akanijibu "Nitaweza!", Sikumwelewa!
Kumbe alikuwa anaona mbali! Alichofanya alichukua hiyo 25,000/= akaenda nayo eneo
moja linaitwa Kalenga (km 7 kutoka Iringa mjini) huko akalima matango. Angalia
mchanganuo: Shamba nusu eka akakodi kwa tsh 10,000/=, mbegu za matango akanunua
tsh. 7,000/=. Kwenye kulima akalima kwa mikono yake akisaidiana na kibarua
mmoja. Fedha iliyobaki 8,000/= akalipa kibarua na kununulia dawa ya kuua
wadudu. Alipokuja kuvuna akapata tsh 800,000/=(laki nane). Alipokuja na fedha
hii tukaenda kutafuta shamba la miti akaanza na ekari moja huku pesa nyingine
akairudisha shambani. Hivi leo Bw. Maganga ana ekari zisizopungua hamsini za
mashamba ya miti na anaendelea na kilimo cha umwagiliaji. Lakini HAPO amefika
kwa kutumia tsh 25,000/= tu. Tunaposema hauhitaji mamilioni kujiajiri
tunatamani ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kama Bw. Maganga. Unaweza
kumwandikia”
Katika makala hii, nimeamua
kuwashirikisha wasomaji wangu kuhusu kilimo cha miti,ambacho ninakifanya mimi
kwa sasa,ili kutunza mazingira na kuilinda dunia na joto.
Kuhusu kilimo cha miti ninacho
kifanya mimi na nimepania kwelikweli ndani ya nchi yangu niipendayo Tanzania ni
kwamba, kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya
mazingira. Katika Tanzania
mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya
kupandwa. Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na
utengenezeaji wa karatasi.
Ukiacha mahitaji haya
tuliyoyazoea; hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya
kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa. Kwa maana hiyo unaweza
kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati
ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea
karatasi. Mbali na kuuza hewa ukaa, vile vile unaweza kufuga nyuki na kuendelea
kuvuna asali wakati unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza miti ya nguzo,
karatasi ama mbao
Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji
wa muda wa kati na mrefu (middle& long term investments). Kiutamaduni
watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu. Hata hivyo kama
una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda
mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa
hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho.
Miti ya mbao inatumia wastani wa
miaka sita hadi 8 au saba, tangu kupandwa hadi kuvunwa kwake. Hii ina maana
inapofikisha umri wa miaka sita huwa tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari
moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti
mmoja kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000,inategemea
na ukubwa wa mti). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa
unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na nane (18,000,000).
Fedha hiyo (kadirio la chini
kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini
kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni
therathini na mbili (32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji(demand) wa
mbao katika soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo
hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi.
Gharama ya kununua shamba tupu ni
kati ya shilingi laki moja na 20 elfu
(120,000) na laki moja,kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata. Gharama
za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi laki moja na nusu,na laki mbili. Hii ina maana kuwa, unaweza
kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu! Kutegemea
na umri wa miti unayotaka.
Mtu unaweza kuona kuwa pengine
kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika na upandaji miti itakuwa ni mlolongo
mkubwa; kukusaidia katika hilo nimekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba
yenye miti (kuuza) kwa bei nafuu sana. Yapo mashamba yenye miti ya kuanzia
mwaka mmoja, miaka miwili, miaka mitatu na miaka minne. Uponunua mashamba haya
kutoka kwangu, mimi naendelea na upandaji wa mashamba mapya kupitia fedha hizo.
Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki
uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika
ukishapanda shamba lako. Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama
karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini.
Kazi namba moja unapokuwa
umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia
moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau
kwa mwaka mara moja (prooning). Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za
moto, kufyekea na kulinda moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima.
Kwa maana hii gharama za
kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni wastani wa
shilingi milioni moja tu. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua
shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.
Hata hivyo nadhani wote
tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile
tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa
ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na
miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha.
Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza
mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa
umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali na hivyo unaweza
ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado una nafasiya kupata faida
hata ndani ya mwaka mmoja, miwili n.k.
Ukishapanda shamba la miti ekari
moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili
hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda
mwingi ama usumbufu wa kusimamia; hakika ni faida nono.
Huenda hadi kufika hapa unaweza
ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa
mawili; “Ninatamani nifanye mradi huu lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?” Pili:
Niko mbali na sina muda wa kushinda Iringa, Je, ni nani atanisaidia kupanda,
kusimamia na kuendesha hayo mashamba?
Ili kutimiza ndoto yangu hiyo nimeweka
utaratibu ufuatao utakaohakikisha kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la
kuwekeza kwenye kilimo cha miti anafanikiwa. Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami
kwa ufafanuzi na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika
kuhusu wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya
uzalishaji katika ardhi yetu. Inawezekana!
Kwa kutumia sheria ya ardhi ya
mwaka 1999 sheria namba 5 utapata documents za umiliki; kwa kuzingatia taratibu
na tamaduni zote za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha
nakusaidia ili ndoto yako itimie.
Yupo Baba yangu anaishi Mafinga
ambae siku za karibuni amepewa Tuzo ya Rais kwa kuwa mpandaji namba moja wa
miti na utunzaji wa mazingira,ameahidi kutoa msaada kwa Mtanzania wa ndani na
nje ya Tanzania kumsadia kupata eneo la kupanda miti na kauli ya siku zote ni “USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA TANZANIA.
No comments:
Post a Comment