Sunday, July 28, 2013

Balozi Modest Jonathan Mero aagwa New York

Mh. Modest J. Mero akipata ukodak wa pamoja na familia yake
Mh. Mero alikuwa anafanya kazi Tanzania Mission New York katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo: Minister Plenipotentiary at United Nations, Minister Plenipotentiary at Government of Tanzania, Partner at PM Consulting Group.

Hivi karibuni Balozi Modest Jonathan Mero aliteuliwa kuwa Balozi mpya wa Tanzania huko Geneva, Uswisi. Jumuia ya Watanzania New York pamoja na Mh. Balozi Tuvako Manongi na wafanyakazi aliokuwa anafanya nao ofisi za Tanzania UN Mission New York walimwandalia BBQ ya kumuaga na kumpa zawadi kama kumbukumbu na heshima kutokana na jinsi walivyo kuwa bega kwa bega katika utendaji wa kazi za kioffice na za kijamii kipindi yupo NYC.

H. E. Mr. Ken Kanda Ambassador & Permanent Representative of The Republic of Ghana
to The United Nations akipata ukodak na Mh. Mero na kushoto kwa Mh. Mero ni mke wake,
anaefuatia ni mke wa Mh. Tuvako N. Manongi Permanent Representative of the United
Republic of Tanzania. Viongozi hao walipata ukodak kumbukumbu mbele
ya Camera ya Vijimambo.

Mh. Balozi Manongi akimsomea maneno yaliyoandikwa kwenye zawadi kabla ya
kumkadhi Mh. Mero
Makamu katibu wa New York Tanzania Community Mariam Abu akimkabidhi zawadi
Mh. Mero kwa niaba ya Community.
Zawadi ziliendelea kama unavyoona
Mh. Balozi Manongi akiongea kabla ya kukabidhi zawadi hiyo, Hafla hiyo ilifanyika nyumbani
kwa Mh. Balozi Manongi , Dobbs Ferry , New York.
Ni zawadi picha kubwa ya ukutani yenye picha ya mama wa Ki-afrika.
Mh. Mero akitoa Shukurani 
Mwenyekiti wa New York Tanzania Community Mr Shaban Mseba akiongea machache
kwa niaba ya Community. Kwa picha zaidi bofya read more













No comments:

Post a Comment