Wednesday, October 2, 2013

Ndoa ya kaka Bakari na Betty katika picha

Bwana na Bi Harusi wakiwa kwenye hisia kali za wapendanao kwenye sherehe ya
 harusi yao iliyofanyika Jumamosi Sept 21, 2013, Hilton Hotel Newark, Delaware
 nchini Marekani na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki kutoka kila
kona ya nchi.
Kwa mara ya kwanza wakiingia ukumbini kama Mke na Mume kwenye sherehe yao ya harusi iliyofanyika Jumamosi Sept 21, 2013 ndani ya Hoteli ya Hilton iliyopo Newark, Delaware.
Maharusi wakisindikizwa na ndugu, jamaa na marafiki kwa shangwe na vifijo huku
maharusi wakinesanesa kwa wimbo wa kabila la Wahaya ambako ndiko
Bwn. harusi anakotokea.Bwn. na Bi. harusi wakiwa meza kuu na wapambe wao
Mchungaji John Mbatta ambaye ndiye baba mzazi wa Bi harusi akiombea chakula
kwenye sherehe ya harusi ya Bakari na Betty iliyofanyika Jumamosi Sept 21, 2013,
Newark Delaware ndani ya ukumbi wa hoteli ya Hilton.

Ndugu wa Bi. harusi kutoka kushoto ni Aunty, Kaka na  Mama mzaa chema
Bwn. na Bi. harusi wakipata chakula.
Wapambe wa maharusi wakipata chakula
 
Mshereheshaji Tuma akiwa kazini.
Juu na chini ni mahahrusi wakicheza dansi yao ya kwanza


Maharusi katika picha ya pamoja na ndugu jamaa na marafiki.
Aunty na Baba mzaa chema wa Bi. Harusi.
Charles Katera akiongea kwa niaba ya wazazi wa Bwn. Harusi.
Madada na kaka wa Bi harusi katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment