Saturday, February 22, 2014

Jumuiya ya Watanzania Houston-Texas (THC) yapata uongozi mpya

Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston, Texas jioni ya leo imepata uongozi mpya wa Jumuiya utakaoiongoza jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka 3. Bi.Nuru Mazora amechaguliwa kwa kishindo kuwa Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo baada ya kupata kura 56 ambazo ni sawa na asilimia 37.1% ya kura zote zilizopigwa akiwaacha wapinzani wake Bw.Erasto Mvungi (kura 39), Bw.Isiah Mgendi (kura 31), Bw. Issa Kingu (kura 19) na Bw.Anthony Ndibahyukao (kura 6).

Bi.Nuru Mazora - Mwenyekiti Mpya ya Jumuiya ya Watanzania Houston (THC)

Naye Bw.Alfred Utatala Nkunga amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo baada ya kumshinda mpinzani wake Bi.Leyla Kikuzi  kwa kupata kura 105 ambazo ni sawa na asilimia 69.5% ya kura zote zilizopigwa kulinganisha na kura 46 alizopata Bi.Leyla.

Bw.Alfred U. Nkunga - Katibu Mkuu mpya wa THC

Uchaguzi huu ulifanyika baada ya uongozi wa Bw.Novatus Simba (Mwenyekiti ) na Bi.Leyla Kikuzi (Katibu) kumaliza muda wake.

VIJIMAMBO  inautakia uongozi mpya wa THC mafanikio mema katika kuwaleta pamoja Watanzania waishio Houston na vitongoji vyake .



No comments:

Post a Comment