Friday, April 25, 2014

Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress amtembelea Balozi Mulamula

Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress akikaribishwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Afisa Ubalozi Suleiman Saleh siku ya Alhamisi April 24, 2014 alipotembelea Ubalozi huo na kujitambulisha kwa Mhe. Balozi Liberata Mulamula (hayupo pichani)
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress kwa Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi huyo alipotembelea Ubalozi huo siku ya Alhamisi April 24, 2014 jijini Washington, DC.
Mhe. Mark Chldress akifanya mazungumuzo na Mhe. Liberata Mulamula siku ya Alhamisi April 24, 2014 alipotembelea Ubalozi huo uliopo Washington, DC na kujitambulisha kwa Balozi.
Mhe. Liberata Mulamula akifanya mazungumuzo na Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Mark Childress.


Mhe. Mark Childress akipokea zawadi toka kwa Balozi Liberata Mulamula
Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Mark Childress akiwa Afisa wa Desk la Tanzania State department Bwn. Nathan Flook.
 Balozi Liberata Mulamula pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakifanya mazungumuzo na Balozi mpya wa Marekani Mhe. Mark Childress akiwa na Afisa wa Desk la Tanzania State Department.
 Picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi

No comments:

Post a Comment