Sunday, June 15, 2014

Usiku wa Wanawake wa Tanzania Wafana

 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwasili kwenye ukumbi wa Martin's Crosswinds uliopo Greenbelt, Maryland kwenye usiku wa Wanawake wa Tanzania ulioratibiwa na kikundi cha wakinamama wa tano chenye maskani yao DMV kinachobeba jina la Tano ladies na kuufanya usiku huo kuwa wa aina yake na kuweka historia ya wanawake nchini Marekani kwa kusahau tofauti zao, kuwaacha wapendwa wao nyumbani na kuwa kitu kimoja kwa kujumuika pamoja kuelimishana juu ya kupendana na kuungana mkono kila mwenzao anapofanya jambo jema.  
Meza alioyokaa Mhe. Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkuu wa Utawala na Fedha, Mama Lily Munanka akijumuika kwenye usiku wa wanawake wa Tanzania uliofanyika siku ya Jumamosi June 14, 2014, Greenbelt, Maryland.


Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea machache kwenye usiku huo na kusisitiza upendo, ushirikiano na mshikamano kwa akina mama na kuwashukuru tano ladies kwa kuja na mawazo ya kuunda kikundi chao kwa lengo la kuwaunganisha wanawake wa Marekani na baadae aliwatunukia zawadi toka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.


Haika Lawere ambaye ni mkurugenzi na mmiliki wa Mbezi Garden Hotel Ltd Tanzania mpenda maendeleo ya akina mama akiongea na kuwaelemisha akina mama juu ya kupendana na kutokuwa na choyo ya kunyimana fulsa za maendeleo na kuwasihi wanawake waache raho za kwanini daima tuwe na wivu wa maendeleo sio wivu wa kurudishana nyuma.


Miriam Kinunda mwandishi wa kitabu cha Taste of Tanzania akielezea sababu za yeye kuandika kitabu chake kwa lugha ya kiingereza kwa kusema sababu kubwa ilikuwa ni kujulisha ulimwengu juu ya mapishi ya Tanzania na kwa kuwa nipo nje ya Tanzania na lengo ya kitabu changu ilikuwa kukiuzwa nje ya Tanzania na akatoa mfano wa Mapishi ya China kama yangekua yanaandikwa Kichina hadhani kama Dunia ingekua inajua mapishi ya Fried Rice.
Juu na chini Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiwazawadia Tano Ladies
Mwenyekiti wa Tano Ladies Asha Hariz akitoa shukurani kwa wanawake wote na kuwashukuru kuwaunga mkono na kukubali wanachofanya.
Asha Nyang;anyi mmoja wa Tano Ladies akiwashukuru wadhamini.
Tano Ladies katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi

No comments:

Post a Comment