Thursday, August 21, 2014

Magwiji wa Tanzania wakijiandaa na mechi ya Real Madrid

Viungo wa timu ya soka ya magwiji wa Tanzania, Athumani China kushoto na Yussuf Macho kulia wakigombea mpira jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya magwiji wa Real Madrid ya Hispania Jumamosi Uwanja huo.

Watu wazima wakipasha leo Taifa. Jumamosi patapendeza Taifa
Kulia Stephen Nyenge, kushoto Boniface Pawasa 'Djanka'
Mohamed Mwameja kushoto akifurahia mazoezi
Kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' kulia akiongoza mazoezi leo, anayepiga mpira ni Shaaban Ramadhani
Sabri Ramadhani 'China' akimiliki mpira mbele ya Yussuf Macho 'Musso'
Watu wazima wakionyeshana kazi katikati ya Uwanja
Wakubwa wameonyesha wako fiti na tayari kuwapa burudani Watanzania Jumamosi

No comments:

Post a Comment