Sunday, September 28, 2014

Misa ya Kumuaga Marehemu Method Mengi yafanyika Houston, TX

Misa ya kumuaga ndugu yetu mpendwa marehemu Method Mengi ilifanyika jana jumamosi katika kanisa Katoliki la StCyril of Alexandria na kuongozwa na Fr.Gerald Singu kutoka Virginia. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuondoka mwanzoni mwa wiki kuelekea nyumbani Morogoro tayari kwa maziko. Pata taswira za Ibada hiyo : 

Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Method Mengi

Fr.Gerard Singu (katikati) kutoka Vurginia akiongoza misa

Mke wa marehemu Method (wa pili kutoka kulia) akiwa kwenye majonzi

Wanajumuia Simon na Michael wakiwasaidi watoto wa marehemu kutoa heshima za mwisho

Jeneza likiingizwa kwenye gari baada ya misa

Gari lililobeba mwili wa marehemu Method

Watoto wa marehemu Method (wa kwanza kulia na wa katikati)

Bw.Michael Ndejembi (rafiki wa marehemu Method) akitoa machache


No comments:

Post a Comment