Thursday, October 2, 2014

DSTV Tanzania yazindua kifurushi kipya

3

Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia), akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba.(katikati), Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi, na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu.

Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania kupitia huduma ya DSTV imewataka wasanii kupeleka kazi zao ili waweze kutambulika nje na ndani ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Furaha Samalu wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba .

Alisema kifurushi hicho mahususi kwa watanzania chenye chanieli zaidi ya 65 za kitaifa na kimataifa zikiwemo za Maisha Magic Swahili inayoonesha filamu za Kiswahili, chaneli ya telemundo, chaneli ya nickelodeoni na Disney junior zinazoonesha vipindi vya watoto.

Alitaja chaneli nyingine zitakazopatikana kwenye kifurushi hicho ni Afrika magic Epic Movie, Discovery world, CBS Action, CBS reality na CBS drama pamoja na Select sport 1 na 2 kwa vipindi vya michezo.

1

Meneja Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Octoba 1,2014 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba.

“Uzinduzi wa kifurushi hichi ni jambo la furaha na msisimko sana kwetu kuona kuwa sasawatanzania wanaweza kupata kifurushi kinachokidhi mahitaji yao.

“Kila wakati multichoice inafanya jitihada za kudumu namna ya kuwapa wateja wetu uwanja mpana wa burudani kwa uwepo wa filamu , makala, habari, vipindi vya watoto, muziki, vipindi vya dini na michezo,” alisema.

Aliongeza kuwa kifurushi hicho kitagharimu kiasi cha shilingi 17,000 kwa mwezi ambapo watakao jiunga watapata DSTV ikiwemo na gharama ya ufundi kwa shilingi 99,000 kwa kipindi maalum.

Alifafanua kuwa kifurushi hicho pia kitawapa fursa watanzania kuangalia Chaneli za Super Sport select1 na 2 ambayo inatonesha ligi kuu ya Uingereza, kombe la klabu bingwa ulaya, ligi kuu ya Hispania, ligi kuu ya Ujerumani pamoja na riadha na ngumi.

2

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa ufafanuzi kuhusiana na kifurushi hicho.

5

Waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi huo.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).

4

No comments:

Post a Comment