Monday, October 13, 2014

Green Waste Pro. yakabidhi msaada Bunge Primary School

DSC_0093

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bunge Bi. Khadija Telela, akizungumza na Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambata na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili (kulia) waliofika shuleni hapo kukabidhi rasmi makasha ya kuhifadhia taka.

Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Usafi ya Green Waste Pro imetimiza ahadi yake ya kuipatia shule ya Msingi Bunge makasha ya kuhifadhia taka na vifaa vya usafi wa mazingira iliyoitoa mwaka jana.

Mwaka jana wakati wanafanya shughuli ya kupaka rangi shule hiyo,kampuni hiyo ilifurahishwa na mazingira ya shule jinsi yanavyotunzwa kiasi cha kufanya maamuzi ya kuwapelekea vifaa vya mazingira na hasa makasha ya kuhifadhia taka.

Kwa mujibu wa Afisa uendeshaji wa kampuni hiyo Abdallah Mbena,ambaye ndiye aliyekabidhi makasha hayo,maamuzi ya kuwapatia makasha yametokana na jinsi klabu ya mazingira ya shule hiyo na mwalimu wao anavyochakarika katika kuhakikisha usafi wa mazingira katika shule hiyo.

Mbena alisema kwamba wamefarijika sana na juhudi zinazofanywa na mwalimu na wanafunzi wake katika kuhakikisha kwamba wanatunza mazingira.

DSC_0076

Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena, akielezea nia ya kampuni yake kuendelea kusaidia shughuli mbalimbali za mazingira katika shule hiyo kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bunge Bi. Khadija Telela (kushoto).

Pamoja na sababu za wanafunzi hao na mwalimu wao katika kutoa kipaumbele mazingira, kuwa chanzo cha kutolewa kwa makasha hayo, sababu nyingine iliyozingatiwa ni kuwa shule hiyo ipo katika kata ya Kivukoni ambapo kampuni hiyo inazabuni ya kufanya usafi.

Amesema wana mpango wa kuwapatia vifaa vya aina hiyo kwa shule nyingine zinazofanya vyema kwenye usafi wa mazingira ila kwa sasa wameanza na shule ya Bunge.

Mwalimu wa mazingira wa shule hiyo, Frida Madanganya ameshukuru kampuni hiyo kwa kuendelea kuwasaidia na anawategemea wataendelea zaidi kuhakikisha kwamba shule hiyo inakuwa namba moja kwa utunzaji wa mazingira.

Naye Mwalimu Mkuu Khadija Telela alisema shule yake ina changamoto kubwa hasa maji ya Dawasco kwani maji yao ni yachumvi kwa kisima walichochimba.

Alisema maji hayo yana chumvi lakini juhudi zinaendelea kupata maji ya Dawasco.

Aidha aliwataka wanafunzi waliosoma hapo kuikumbuka shule hiyo kwani wengi wana uwezo wa kuifanya iendelee kuwika.

DSC_0058

Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwalimu Frida Madanganya akiwatembeza kukagua mazingira ya maeneo mbalimbali ya shule hiyo Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili kabla ya kukabidhi makasha hayo.

DSC_0046

Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwl. Frida Madanganya akimtambulisha Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena kwa wanachama wa klabu ya mazingira wa shule hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi makasha ya kuhifadhia taka.

DSC_0053

Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena akizungumza na wanafunzi wa klabu ya mazingira shule ya msingi Bunge na kuwahamasisha kuendelea kutunza mazingira yao na hata majumbani pia ili wawe mabalozi wazuri wa mazingira.

DSC_0024

Kaka Mkuu wa shule ya msingi Bunge na mwenyekiti wa klabu ya mazingira shuleni hapo Joseph Zakayo (kulia) akitoa shukrani kwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd kwa kutoa msaada huo wa makasha matatu ya kuhifadhia taka. Kushoto ni Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwl. Frida Madanganya akifuatiwa na Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.

DSC_0062

Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena akikabidhi rasmi moja kati ya makasha matatu ya kuhifadhia taka yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwl. Frida Madanganya. Kulia ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.

DSC_0003

Baadhi ya michoro iliyopo kwenye majengo ya shule ya msingi Bunge yanayohamasisha utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa shule hiyo.

DSC_0102

Wanafunzi wa klabu ya mazingira shule ya msingi Bunge wakiagana na Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.

No comments:

Post a Comment