Tuesday, November 18, 2014

Skymoto Band yawabamba wakazi wa Mwanza

DSC_0206

Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band Dkt. Sebastian Ndege a.k.a JembeniJembe akizungumza na wakazi wa Mwanza kuwakaribisha kwenye show ya SKYMOTO iliyofanyika kwenye hekalu la maraha la Jembe Beach lililopo Malimbe jijini Mwanza.

DSC_0209

Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band Dkt. Sebastian Ndege a.k.a JembeniJembe akimtambulisha Mkurugenzi wa Yamoto Band Said Fella almaarufu kama Mkubwa na wanawe kwa wakazi wa jijini Mwanza waliotinga kwenye hekalu la maraha lililo Malimbe jijini Mwanza Jembe Beach.

DSC_0119

Vijana wa Skylight Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza wakifungua burudani kwa kumpa sapoti Digna Mbepera (wa pili kulia) kutoa burudani kwa wakazi na mashabiki wa Skylight Band mwishoni mwa juma. Kutoka kushoto ni Sony Masamba, Aneth Kushaba AK47 pamoja na Hashim Donode (kulia).

DSC_0015

Divas wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 na Digna Mbepera wakionyesha ufundi wao ndani ya Jembe Beach.

DSC_0127

Rapa mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower (kushoto) akiongoza kikosi cha Skylight Band kutoa burudani kwa wakazi wa jijini Mwanza kwenye show ya aina yake iliyopewa jina la SKYMOTO huku wakikolabo na Yamoto Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza.

DSC_0131

Raia wa kigeni na couple yake wakiburudika na burudani kutoka vijana wa Skylight Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza.

DSC_0098

Kikosi kazi cha Skylight Band kikishambulia jukwaa kwa manjonjo ya aina yake.

DSC_0142

Sam Mapenzi wa Skylight Band akiwa raha wakazi wa jijini Mwanza ndani ya Jembe Beach mwishoni mwa juma walipo kolabo na Yamoto Band.

DSC_0144

DSC_0163

Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na Skylight Band ndani ya Jembe Beach.

DSC_0175

DSC_0185

DSC_0187

DSC_0195

Aneth Kushaba AK47 akiwa chezesha ligwaride wakazi wa Mwanza ndani ya Jembe Beach.

DSC_0016

Sam Mapenzi, Aneth Kushaba na Digna Mbepera wakishambulia jukwaa.

DSC_0036

Pichani juu na chini ni sehemu ya wakazi wa jijini Mwanza waliofurika kwenye show ya SKYMOTO ndani Jembe Beach.

DSC_0135

DSC_0213

DSC_0020

Dogo Asley akiongoza Yamoto Band kutoa burudani kwa wakazi wa jijini Mwanza walipofanya kolabo na Skylight Band kuwapa raha wakazi wa jijini Mwanza.

DSC_0026

Yamoto Band wakishambulia jukwaa ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza mwishoni mwa juma.

DSC_0034

Yamoto Band wakitoa burudani kwa wakazi wa Mwanza ndani ya Jembe Beach.

DSC_0052

Yamoto wakimwaga mauno kwa mashabiki wa wakazi wa jijini Mwanza ndani ya Jembe Beach.

DSC_0009

Wadau wengine watulia karibu na kaunta ya vinywaji ya Jembe Beach huku wakiburudika na burudani ya Skylight Band kwa mbali wakichochea mzuka wa kucheza.

DSC_0215

Pichani juu na chini mashabiki wakiwa wamefurika kenywe bustani ya Jembe Beach kushuhudi burudani ya Live Music kati ya Yamoto Band na Skylight Band show ya iliyopewa jina la "SkyMoto" maalum kwa mashabiki wa jijini Mwanza.

Kwa picha zaidi ingia hapa

No comments:

Post a Comment