Maafisa wa polisi mjini NORTH Carolina nchini Marekani wamemkamata
mtu mmoja baada ya wanafunzi watatu waislamu kupatikana wamefariki
nyumbani mwao.
Miili ya Deah Barakat,mkewe Yusor Mohammed Abu salha na dadaake Razan
Mohammed Abu salha ilipatikana siku ya jumanne ikiwa na majeraha ya
risasi katika vichwa .
Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 46 tayari amefunguliwa mashtaka kutokana na mauaji hayo.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kubaini iwapo mauaji hayo yanatokana na chuki.
Swala kwamba wanafunzi waliouawa ni waislamu limezua uvumi katika mitandao ya kijamii wa iwapo mauaji hayo ni ya kidini au la
Uchunguzi uliofanywa umebaini kwamba uhalifu huo ulitekelezwa kutokana
na mzozo unaondelea kuhusu uegeshaji wa magari,maafisa wa polisi wa
Chapell wamesema.
No comments:
Post a Comment