Friday, March 13, 2015

PAZI REUNION MAMBO YAZIDI KUPAMBA MOTO HOUSTON, TEXAS


 Watatu toka kushoto ni Richard Kasesela alipokua akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa George  Bush Intercontinental uliopo Houston, Texas nchini Marekani kwa ajili ya Pazi Reunion itakayofanyika siku ya Jumamosi March 14, 2015 katika uwanja wa mpira wa kikapu wa Pilgrim uliopo katika kanisa la Lutheran lililopo Houston. Wengine katika picha ni wenyeji wake waliompokea,  kutoka kushoto ni Willy Crrusa, Aika na Flora Mochiwa maarufu kama Madikodiko. Mchezaji mwingine anayekuja kwenye maadhimisho hayo ya Pazi toka nje ya Marekani ni Atiki Matata anayekuja siku ya Ijumaa March 13, 2015 akitokea Uingereza. Picha na VIJIMAMBO
 Richard Kasesela akitest uwanja wa mpira wa kikapu mara tu alipowasili uwanjani hapo mara tu baada ya kutoka uwanja wa ndege kushoto ni Davis mchezaji mwingine wa mchezo huo, Flora Mochiwa na Willy Crrusa wakiangalia kama bado wamo. Richard Kasesela richa ya kuwa mchezaji wa Pazi pia aliwahi kuwa Rais wa chama cha mpira wa kikapu Tanzania.
 Wachezaji wa mpira wa kikapu wakipata picha ya pamoja na Richard Kasesela.
 Mdau toka Columbus, Ohio akiwa tayari kushuhudia Pazi Reunion itayaofanyika siku ya Jumamosi March 14, 2015 ndani ya jiji la H-Town.
 Willy Crrusa katika picha ya pamoja na Andrew wakati wakiwa ndani ya madikodiko.
 Wageni wakipata chakula huku maongezi yakiendelea.
Andrew akipata picha ya pamoja na Richard Kasesela.

No comments:

Post a Comment