Friday, March 6, 2015

Ushirikina Chanzo cha Mauaji ya Albino

Na Andrew Chale wa modewji blog
Dk. Ally Possi ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam. Akielezea na kuchambua kwa kina kuhusiana na wimbi la mateso na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wenye albinism.
Mo dewjiblog, iliamua kufanya mahojiano maalum ilikukuletea wewe msomaji wetu unayeperuzi mtandao wako bora kabisa kujua na kuelewa na nini kifanyike ikiwemo mimi na wewe katika kuchukua hatua.
Suala la mauaji dhidi ya watu wenye albinism:
“JAMII yenye ushirikina ndio yenye kuamini suala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambao wana albinism, hivyo ilikuondoa imani hii potofu ni kutoa elimu katika maeneo yote na kuwalinda popote pale, Jambo hili ni jukumu letu sote” anabainisha Dk. Ally Possi.
Dkt. Possi anabainisha kuwa, Serikali itaendelea kulaumiwa mpaka hapo juhudi za dhati za kukomesha mauaji na vitendo vya kikatili vitakavyochukuliwa na kutokomezwa kabisa.
Fuatilia hapa Mahojiano hayo maalum.
DSC_0391
Mwanasheria na mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dk. Ally Possi akiwa kwenye ofisi za modewjiblog kabla ya mahojiano na mtandao huu.
MO DEWJI BLOG : Karibu, mgeni wetu katika mtandao huu wa kijamii unaokuletea habari bora kabisa zilizochambuliwa kwa kina za ndani, nje na makala maalum za kina.
DK. POSSI: Asante, nashukuru sana…
MO DEWJI BLOG: Unadhani nini chanzo na hali ya ongezeko la vitendo hivi kwa sasa hapa Tanzania?
DK.POSSI: “Kwanza mauaji ni.. yanatokana na imani potofu. Imani potofu kwa jamii kuwa ukipata kiungo cha alibino unafanikiwa.
Hii ni imani potofu kwa jamii ya watu wenye kuamini ushirikina.
“Albino ni ulemavu ambao mtu anakosa aina ya vitamin inayoitwa melaniani…
Inakosekana ikiwemo katika ngozi, nywele na macho” anaendelea kubainisha kuwa: Kuwa albinism ni hali ya kurithi kutoka kwa wazazi wote wawili ama mmoja. Ni kwamba baba na mama wanakuwa na vinasaba vinavyokuwa na albinism na vinapokutana wakati wa kutunga mtoto ndipo mtoto mwenye albinism anazaliwa.
MO DEWJI BLOG: Vipi inahusishwa na suala la Imani?
DK. POSSI: “Imani sio dini, Ni imani ya kishirikina.
“Sijui kitu gani ambacho kimetokea kikaleta hiyo imani, kwa kifupi ipo kwenye jamii iliyoendelea na uwezo wake wa kiuchumi ni mdogo na elimu pia.
Pia tunaweza kusema: “Suala hili ni la imani, Imani si ya dini, bali ni ya kishirikina. Kwa sababu kuna mtu anasema yeye muislamu ama mkristo.
Au kuna mtu ana Phd/ Profesa, ama amesoma elimu nzuri tu ama ana pesa anafanya biashara au mfanyabishara au mwanasiasa mwenye elimu yake nzuri lakini ametumbukia kwenye imani hii ya kishirikina.
DSC_0355
Mwanadishi wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale akiwa kwenye mahojiano maalum na Dk. Ally Possi.

MO DEWJI BLOG: Kwa nini Kanda ya ziwa mauaji haya yamezidi kwa kasi?.

Dk. POSSI: “Kwanza kuna tatizo: Ofkozi..mauaji hayo Kanda ya ziwa mauaji yameripotiwa sana pia kuna Morogoro pia na sehemu nyingine.
“Serikali imekuwa kimya sana… katika mauaji yametokea husikii kiongozi mkubwa, ukiondoa Rais alivyosema (Machi 2-wakati wa hotuba ya mwisho wa mwezi wa Februari), lakini kiongozi mkubwa wa juu Waziri Mkuu, tangu mtoto Yohana yule wa Geita, Chato kukutwa ameuwawa
Sijasikia kauli nyingine zaidi ya Rais…Ambayo nayo ameitoa wiki mbili hadi moja na nusu, kupita ndio Rais anatoa tamko hilo.
“Nafikiri Serikali imekaa kimya kutoa matamko ama imekuwa ‘slow’ kuchukua maamuzi ama hatua stahiki hasa kwa watuhumiwa huko vijijini.
“Sote tumekaa vijijini ama tuna ndugu vijijini, Mtu anaweza kuibaa Baiskeli kijijini lakini masaa tu, anakamatwa. Lakini watuhumiwa wale wa vijiji wa mauaji ya watu wenye albinism kwa nini ichukue muda wasikamatwe?.
MO DEWJI BLOG: Tuambie inakuaje katika suala la kisheria?.
Dk. POSSI: “Sidhani kama kuna kitu kigumu kuwachukua watuhumiwa vijijini, wakati mtu akiiba baiskeli baada ya muda anakamatwa. Hapa nadhani suala la kisheria lipo kwa watu wote. Sheria inabidi ichukue mkondo wake kwa kuchukua maamuzi stahiki na ya haraka katika kuyafanyia kazi ikiwemo kuwakamata watuhumiwa popote walipo.

No comments:

Post a Comment