Sunday, April 17, 2016

SIMBA NA YANGA UGHAIBUNI SASA KUCHEZA DALLAS, TEXAS KWENYE KONGAMANO LA DICOTA

Kikosi cha Simba.
Kikosi cha Yanga
 
Aliyekua mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka akisalimiana na wachezaji wa Yanga ambao ndio walichukua kombe la DICOTA mwaka 2011 ilipofanyika Washington, DC.
Aliyekua mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka akisalimiana na wachezaji wa Simba.

Siku ya Jumamosi April 30, 2016 itakua historia kujiludia pale mpambano wa Simba na Yanga utakapoandika ukurasa mpya kwa mara ya kwanza kuchezewa Dallas, Texas.

Mpambano huo unaosubiliwa na mashabiki watakaohudhuria DICOTA kutoka Tanzania wakiwemo watakaotoka majimbo mbalimbali Marekani, ni mpambano utakaoandika historia mpya na kwa mara ya kwanza pambano hilo kuchezewa Dallas, Texas.

Mpambano huo utakaoenda sambamba na nyama choma ikwemo michezo ya watoto, mpira wa kikapo na mpira wa wavu, unatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Huffhines Recreation Center anuani 200 N Piano Road, Richardson, TX 75081 na mechi inatarajiwa kuanza saa 10 jioni (4pm).

Mechi ya Simba na Yanga itakuwa wazi kwa kila shabiki kucheza na kila shabiki kushangilia. Mpambano wa Simba na Yanga uliofanyika Washington, DC Octoba 16, 2011 Yanga iliibuka mshindi wa kombe hilo la DICOTA baada ya kuibamiza Simba kwa bao 6-4 baada ya dakika 90 timu hizo kufangana bao 4-4 na kuongezwa muda wa nyongeza dakika 15 kila kipindi.

No comments:

Post a Comment