Monday, December 12, 2016

DINNER YA JUMUIYA YA WATANZANIA COLUMBUS, OHIO (MFUKO)

Vera Teri - Mwenyekiti ya Jumuiya ya WaTanzania Columbus, Ohio nchini Marekani akitoa neno la shukurani kwa WaTanzania waliohudhuria halfa ya chakula cha jioni siku ya Jumamosi Desemba 10,2016 iliyoandaliwa na viongozi wa Jumuiya hiyo inayojulikana kama (MFUKO) katika kuadhimisha miaka ya 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Jumuiya hiyo ambayo mpaka sasa inawanachama hai zaidi ya 80 wengi wao wakiwa  wakazi wa Columbus, Ohio. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production.Abraham Aziz - Katibu wa Jumuiya ya WaTanzania akielezea majuisho ya jumuiya hiyo zikiwemo changamoto zake na kutoa wito wa wanajumuiya hiyo kuendelea kuwashawishi wanajumiya wengine ambao sio wanachama wajiunge kwenye MFUKO wa jumuiya hiyo kusudi likiwa ni kuapanua wigo wa kusaidiana kwenye nyanja mbalimbali tofauti na ilivyozoeleka kwa sasa ya Jumuiya hiyo kuchangiana kwenye majanga ya misiba.

Mshereheshaji wa hafla hiyo ya chakula cha jioni Bwn. Peter Kirigiti akielezea jambo.
Theresia Mkangara - Mjumbe wa Jumuiya hiyo akiongoza wimbo wa Taifa
Wanajumiya wakiimba wimbo wa Taifa.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Wanajumuiya wakifanya dua.
Wakati wa chakula.
Mshindi kwenye shindano la watoto la ufahamu wao lugha ya Kiswahili akionyesha zawadi yake.
 Mshindi shindano moja ya shindano kwa wakubwa akionyesha zawadi yake.
 Washindi waliochuana mpaka mwisho wa maswali ikabidi wote wazawadiwe zawadi za ushindi.
Mshindi wa moja ya shindano lililofanyika kwenye hafla hiyo ya chakula cha jioni.

viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Columbus ambao ni Vera Teri - Mwenyekiti, Abraham Aziz - Katibu, Metty Nyang'oro - Mweka Hazina, Halima Salehe - Mjumbe, Hildegard Kamazima - Mjumbe, Rashid Omar - Mjumbe, Emmanuel Mshiu- Mjumbe na Theresia Mkangara - Mjumbe wakiwa katika picha ya pamoja.


No comments:

Post a Comment