Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston , Texas siku ya Jumamosi tarehe 04/22/2017 walifanya kumbukumbu ya kutimia kwa mwaka mmoja tokea mwanajumuiya mwenzao Bw. Andrew Nicky Sanga alipofariki dunia. Shughuli hiyo iliyohudhuriwa na watanzania wengi kutoka jimbo la Texas na majimbo mengine ya hapa Marekani ilianza kwa ibada fupi iliyoongozwa na Rev. Godwin Chilewa iliyofanyika kwenye eneo ambalo marehemu Andrew alipata ajali.
Baada ya ibada wanajumuiya walikutana kwa chakula cha usiku na vinywaji katika ukumbi wa
7 Star Cafe uliopo 14144 Westheimer Rd. Houston Texas 77077
Pata picha za tukio hilo hapa chini :
|
Mama mtoto wa marehemu Andrew, Emmy akiwa na bint wao Zoe |
|
Wanajumuiya wakiwa katika ibada |
|
Marafiki wa karibu wa marehemu Andrew kushoto ni Deo Temba na Wash Drew |
|
Dr. Jenga, John na Re. Chilewa |
|
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Bw. Daudi Mayocha akizungumza |
No comments:
Post a Comment