Katika ziara hiyo pia Mh. Balozi Masilingi alikutana na familia zilizoathirika na kimbunga cha Harvey ambacho kililikumba jiji Jimbo la Texas mwezi Agosti mwaka huu. Mh. Balozi Masilingi vilevile alikabidhi mchango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa familia hizo ambazo zilipoteza mali na wengine makazi wakati wa kimbunga.
Mkutano na Wanajumuiya wote ulifanyika katika Ukumbi wa Hotel Marriott uliopo Briarpark Dr. Houston, Texas . Pata picha za mkutano huo hapa chini.
Mh. Balozi WIlson Masilingi akiongea na wana-Houston |
Mh. Balozi Masilingi akiwasalimia Watanzania wa Houston |
Rai wa Jumuiya ya Watanzania wa Houston (THC) akimkaribisha Mh. Balozi Masilingi |
Mh. Balozi Masilingi akiwa na Rais wa THC Bw. Mayocha |
Viongozi wa THC wakiwa na Mh. Balozi Masilingi, kutoka kushoto ni Bw. Lambert Tibaigana (THC Vice President), Mh. Balozi, Bw. Mayocha (THC President) na Bw. Cassius Pambamaji ( THC Spokesperson) |
No comments:
Post a Comment