Monday, October 17, 2022

AFCON HOUSTON 2022: TANZANIA MABINGwA WAPYA , DRC YALALA 1-0

Tanzania jana jioni ilitwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Africa (AFCON) kwa wana DIASPORA wanaoishi katika Jiji la Houston Jimboni Texas Marekani baada ya kuilaza DRC 1-0 kwenye mchezo mkali wa fainali.

Bao pekee lililopeleka nderemo na chereko kwa mashabiki lukuki waliohudhuria fainali hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Cullen Park lilifungwa na kiungo mshambuliaji Kiswaby "De Bruyne" Maswaga kwa shuti kali katika dakika ya 78 ya mchezo baada ya kupokea pasi safi ya mshambuliaji hatari Rashid Mayele ambaye kabla ya kumpasia mfungaji alikuwa amepokea pasi safi kutoka kwa Ally Ngolo Messi

Baada ya goli hilo timu zilishambuliana kwa kasi lakini hadi kipyenga cha mwisho kinapulizwa na refarii Lee Smith Tanzania waliibuka wababe.

Mbali na zawadi ya kikombe na medali Tanzania ilipokea hundi ya $1000 kama zawadi ya mshindi wa kwanza.

Tanzania pia ilizoa zawadi nyingi zikiwamo hizi;

Top Scorer - Rashid Bulele Mayele ( 9 goals)

Best Player - Kisuby De Bryne Maswaga

Best Goalie - Bita Valante 

Best Coach 


Kisuby De Bruyne Maswaga mfungaji wa bao pekee


No comments:

Post a Comment