Friday, January 27, 2023

YANGA NA SIMBA UGHAIBUNI KUNOGESHA OLD SCHOOL REUNION JUNE 17, 2023 DMV

Timu ya Yanga Ughaibuni

Timu ya Simba Ughaibuni


Na Mwandishi wako kutoka Washington, DC

Mtanange wa Yanga na Simba Ughaibuni utafanyika Jumamosi ya June 17, 2023 DMV.Ttimu hizi zinazoundwa na mashabiki wa timu hizi na baadhi ya wachezaji waliochezea timu hizi zamani huwa na msisimko wa kipekee na yote ni katika kunogesha BASH kubwa la aina yake la Old School Reunion ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka.

Tamasha hili la Old School Reunion halikufanyika kwa miaka 2 mfululizo kutokana na Dunia kukumbwa na Janga la Uviko-19. Mara ya mwisho tamasha hilo kufanyika ilikua mwaka 2019 Jijini Houston, Texas na Yanga ikiambulia kichapo kizito cha mabao 4-1 kutoka kwa mahasimu wao Simba SC

Old School Reunion hukutanisha vijana wa zamani kutoka kila pembe ya Dunia na kukumbuka enzi zile walizokuwa wakiruka majoka na burudani hii huletwa kwenu na MaDJ mahiri wa Old School nchini Marekani, Dj Luke Joe akishirikiana kwa karibu na Dj Dennis (ThaFunkHouse) katika kuhakikisha moja na mbili haiendi kombo.

Old School Reunion ya mwaka huu inatarajiwa kuwa ya aina yake kutokana kwamba haijawahi kutokea ndani ya miaka miwili na pia kuna uwezekano wa kupata wageni mashuhuri kutoka Tanzania kwa sasa ni mapema sana kutaja majina yao lakini kadri muda utakavyokaribia majina yao yatajulikana.

Old School Reunion inatarajiwa kufanyika katika ukumbi waWest Bowie Village Hall mara tu baada yaa mtanange wa Yanga na Simba. Taarifa zaidi zitafuata.Kkaribuni sana katika Jiji la watunga sheria.
No comments:

Post a Comment