Sunday, March 18, 2012

SIMBA SC 2, MTIBWA SUGAR 1

Wachezaji wa SC wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Patrick Mafisango.

Emmanuel Okwi akijaribu kumtoka beki wa Mtibwa Sugar, Juma Jafari

Golikipa wa Mtibwa Sugar, Deogratius Munishi akishika nyavu kwa uchungu baada ya kufungwa bao la kwanza

 
Haruna Moshi 'Boban' akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Salvatory Ntebe (kushoto)

SIMBA SC imeendelea kushika usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo, baada ya kuinyuka Mtibwa Sugar mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Magoli ya Simba yamefungwa na Patrick Mafisango na Felix Sunzu, wakati bao la Mtibwa likiwekwa kimiani na Hussein Javu. Kwa ushindi huu Simba SC wamefikisha pointi 47 wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 44 na Yanga SC yenye pointi 43.

1 comment: