Friday, June 8, 2012

AUAWA NA KISHA KUNYOFOLEWA UUME, NA MIKONO MKOANI ARUSHA


KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA ARUSHA LIBERATUS SABAS 

 Mtu mmoja ambaye hajajulikana jina lake amefariki dunia huku baadhi ya viungo vyake hasa sehemu za uume wake zikiwa zimechomolewa pamoja na mikono yake
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa arusha Sabas Liberatus alisema kuwa tukio hilo lilitokea may 26 majira ya saa tano asubuhi katika eneo la Mto Nambala wilayani Arumeru
Kamanda Sabas alisema kuwa katika siku ya tukio mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume ambaye hajatambulika mpaka sasa anakadiriwa kuwa na miaka 25-30 alikutwa akiwa amefariki
Kamanda huyo aliongeza kuwa mara baada ya wapita njia kumkuta akiwa amefariki waligundua kuwa pia hana viungo mbalimbali ndani ya mwili wake hali ambayo ilizua tafrani kubwa
‘hawa watu walipomuangalia kwa undani sana waliweza kujua na kutambua kuwa baadhi ya viungo vyake havipo na ndipo walipota taarifa kwa jeshi la polisi na sisi tulipoofika ndani ya eneo la tukio tuliyakuta hayo hayo”alisema Kamanda Sabas
Pia aliongeza kuwa baada ya polisi kufika katika eneo la tukio walikuwa mwili huo ukiwa na suruali aina ya jeans ambayo ilikuwa imeshushwa hadi chini ya magoti na viungo vyake vikiwa vimenyofolewa
Hata hivyo jeshi hilo linaendela na upelelezi juu ya tukio hilo na upelelezi wa kufahamu chanzo cha mauaji hayo huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mount Meru

No comments:

Post a Comment