Saturday, June 9, 2012
CCM WAZUNGUMZIA MIRADI YA MAENDELEA JANGWANI LEO

 Waziri wa Ujenzi Mh.John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano wa wachama wa CCM Jangwani leo jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya mikakati ya chama kusikiliza kero za wananchi pamoja na mfumuko wa bei na upandaji holela wa nauli na kuelezea miradi mbalimbali inayoendelea nchini
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE) 
Waziri wa uchukuzi Mh.Harrison Mwakyembe akihutubia katika mkutano wa wachama wa CCM jangwa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mikakati ya chama  kusikiliza kero za wananchi pamoja na mfumuko ya bei na upandaji holela wa nauli na kuelezea wananchi miradi mbalimbali inayoendelea 
 Katika picha kutoka kushoto ni mawaziri Prof Anna Tibaijuka, John Magufuli na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam John Guninita.
 Abdulrahman Kinana (kulia) akipeana  mkono na waziri John Magufuli kushoto.


 Wanachama wa CCM wakichambua baadhi ya kadi ya vyama pinzani zilizorudishwa na wanachama wao kama zinavyoonekana katika picha
 Waziri wa nyumba na maendeleo na makazi Profesa Anna Tibaijuka akifafanua jambo katika mkutano huo
Viongozi wa CCM pamoja na mawaziri wakiimba katika mkutano huo uliofanyika Jangwani jijini Dar es salaam leo

No comments:

Post a Comment