Friday, June 22, 2012


Emmanuel Okwi.
KLABU ya Orlando Pirates ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili kiungo mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, raia wa Uganda.
Okwi anatarajiwa kwenda nchini Afrika Kusini wiki ijayo ili kukamilisha mchakato wa usajili wake ambao utaigharimu Orlando Pirates kiasi cha randi milioni 7 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 190.
Mganda huyo ambaye alichangia kuipa Simba ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita, aliwahi kufanya majaribio klabuni hapo msimu uliopita na alikuwa ameitwa tena kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo kwa mara ya pili.
Gazeti moja la michezo la Afrika Kusini limemnukuu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga: “Kila kitu kimekamilika lakini kuna vitu vichache ambavyo tunatakiwa kukamilisha kabla hatujamruhusu rasmi Okwi.
“Okwi alikuwa msaada mkubwa kwenye klabu yetu kutwaa ubingwa wa ligi kuu (Bara) msimu uliopita, ulikuwa ni uamuzi mgumu kumruhusu aondoke, lakini tuna furaha na tunamtakia neema huko aendako.”

No comments:

Post a Comment