Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya

KLABU ya Bayer Leverkusen imeitupilia mbali ofa ya Chelsea kwa mshambulaji wao mwenye umri wa miaka 21, Andre Schurrle.
KOCHA Alan Pardew amesema kwamba anafanya kila atakachoweza kuhakikisha anambakiza mshambuliaji Demba Ba, mwenye umri wa miaka 27, katika klabu ya Newcastle.
Daniel Sturridge
Spurs inamtaka Daniel Sturridge
TOTTENHAM Hotspur inataka kutoa dai la pauni Milioni 5 kumsajili mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22, Daniel Sturridge wa Chelsea.
KIUNGO wa Arsenal, Aaron Ramsey, mwenye umri wa miaka 21, amesema kwamba yeye na wachezaji wenzake hawajui mambo yatakuwaje mshambuliaji wao Robin van Persie akiondoka.
KOCHA wa Swansea City, Michael Laudrup anajaribu kumsajili winga wa Bristol City, Albert Adomah kutoka Ghana mwenye umri wa miaka 24, usajili ambao unaweza kumgharimu pauni Milioni 3.
KOCHA Roberto Mancini yupo karibu kusaini mkataba mpya na Manchester City, licha ya Chama cha Soka Urusi kutenga kitita kizito kujaribu kumnasa.
KLABU ya Liverpool imekula za uso tena, baada ya kukataliwa kuuziwa kiungo mwenye umri wa miaka 25, Esteban Granero na Real Mdrid.
KLABU ya AC Milan imesema ni bora kumchukua kwa mkopo kuliko kumnunua jumla mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23.
KLABU ya Fiorentina inamtaka mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco, Marouane Chamakh, mwenye umri wa miaka 28, ambaye anajiandaa kuondoka Arsenal baada ya mambo kumuendea ovyo.
KOCHA wa Wigan, Roberto Martinez anamtaka winga wa Chicago Fire, raia wa Guatemala, Marco Pappa, mwenye umri wa miaka 24 azibe nafasi ya mchezaji anayetakiwa na Chelsea, Victor Moses.
KLABU ya Arsenal nayo ipo kwenye mkakati wa kumnunua mchezaji wa Wigan, Victor Moses, mwenye umri wa miaka 21.
KLABU ya Norwich imetoa ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Canaries, James Vaughan, mwenye umri wa 23, kwa Birmingham kuwasaidia kumbakiza beki wa kati, Curtis Davies, mwenye umri wa miaka 27.
KIKOSI cha Tottenham Hotspur sasa kipo kamili chini ya kocha mpya, Andre-Villas Boas, kwa mujibu wa Danny Rose, mwenye umri wa miaka 22.
KOCHA Roberto Mancini aliepuka mapokezi wakati kikosi cha Manchester City kilipowasili katika kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Austria, kulingana na tetesi zinazozagaa kuhusu mustakabali wake.
MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Edin Dzeko ameungana na mwigizaji nyota wa Hollywood, Angelina Jolie katika zuli jekundu kwenye tamasha la filamu mjini Sarajevo.