Sunday, July 15, 2012

Houston yaitupia Wichita 3-1 leo hii huko Wichita , KansasTanzania-Houston Team

Ikicheza kandanda safi na hali ya juu Team ya TZ-Houston imeendeleza wimbi la ushindi wake wakiwa nje ya mji wao baada ya kuibanjua team ya Wichita bao 3-1!
 
Peter Bategeki
Ally Mtumwa

Peter Bategeki akifunga mabao 2 na Ally Mtumwa akipiga la 3 na kuzima kabisa tambo za wenyeji kama watashinda pambano hilo!

Houstonians wanarudi nyumbani kesho jioni!
 

Wakati huohuo
 
Timu ya South Sudan imeomba mechi ya kirafiki na TZ-Houston siku  Jumamosi tarehe 07/21/2012 kwenye viwanja vya Bellaire ktk sherehe za kutimiza mwaka mmoja toka nchi yao ipate Uhuru!

South Sudanese waliopo USA wameichagua Houston kama ndiyo host kwenye sherehe zao kwa hiyo team tutakayocheza nayo ni South Sudanese wote waliopo USA na tukumbuke kuwa South Sudan waliopo Houston walitufunga bao 5-4 kwenye mashindano yaliyopita ya African Cup!

Baada ya mechi hiyo kutafuatiwa tafrija ya kusheherekea uhuru wao kwenye ukumbi wa I-6 na sisi tumealikwa kwenye sherehe hizo!

Kwa vile kutakuwa na mambo mengi siku hiyo na michezo mbali mbali kabla ya soka game basi mechi yetu itaanza saa 10 jioni!

Msemaji wa team

Baba Aggy aka Kindic

No comments:

Post a Comment