Sunday, July 8, 2012


Mabadiliko ya Jina la Tawi - CCMTexas


Ndugu wanaCCM,


Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Tawi la Marekani kilichokutana Houston
tarehe 13.03.2012, pamoja na mambo mengine kilijadili haja na hoja ya kuwa na
matawi kila State za Marekani ili kurahisisha utendaji wa shughuli za Chama.

Kwa minajili hiyo sisi wanaCCM wa Jimbo la Texas tumeitikia wito huo na tayari 
tumebadili jina kutoka CCM Marekani kwenda CCM-Texas.Jina hili jipya 
linatuonyesha uhalisia ya pale tulipo tofauti na la awali ambalo lilijumuisha Marekani yote.

Tumeshaunda uongozi wa muda wa Tawi la CCM-Texas ambalo litakuwa na 
mashina ya Houston na Dallas.

No comments:

Post a Comment