Wednesday, July 18, 2012

MATUKIO YA UOKOAJI WA WATU WALIOZAMANA NA MELI YA MELI YA STAR GATE HUKO KATIKA BAHARI YA CHUMBE ZANZIBAR

 Meli ya Mv Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar
 imezama majira ya saa nane mchane hivi leo katika maeneo Pungume na
 Chumbe baada ya kukumbwa na upepo mkali.

Meli hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana imepindukia
 upande mmoja na huku abiria wengi wakiweza kuokolewa kutokana na 
jitihada mbali mbali kupitia vile vile msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, 
Tug ya Bandari na vyombo vyengine.

Mpaka tunandika taarifa hizi ni maiti tatu zilikwishapatikana na 
kiasi cha abiria 150 wameokolewa na waliojeruhiwa wanatibiwa 
katika Hospitali ya Mnazimmoja. Taarifa zinaeleza kwamba 
kulikuwa na watoto takriban 30 na Watalii kutoka nchi mbali mbali 
wafikao kumi.

Wazamiaji kutoka Kikosi cha KMKM pamoja na Jeshi tayari wapo
 eneo la ajali kusaidia kuokoa maisha ya wananchi waliokumbwa 
na maafa haya. 
 Majeruhi alieokolewa 
katika meli ya StarGate 
iliozama huko katika bahari 
ya Chumbe Zanzibar na 
ikiwa na abiria 250. 

No comments:

Post a Comment