Friday, July 20, 2012

CCM-Texas : Salamu za Rambirambi Ajali ya MV.SkagitChama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Jimbo la Texas kimepokea kwa masikitiko taarifa za ajali ya Meli ya MV.Skagit iliyotokea siku ya jana karibu na kisiwa cha Chumbe.

Kwa masikitiko makubwa tunawapa pole wale wote waliopoteza ndugu , jamaa na marafiki katika ajali hiyo na kuwatakia heri majeruhi wote wapate kupona mapema na kurudi kwenye shughuli zao za ujenzi wa Taifa.

 
MV.Skagit baada ya Ajali


Kwa taarifa tulizonazo ni kwamba mpaka sasa idadi ya waliopoteza maisha kwenye ajali ya MV.Skagit ni 68 ambapo baadhi ya maiti tayari zimetambuliwa na tayari majeruhi zaidi ya 100 walikua wamefikishwa hospitali huku watu ambao hawajaonekana wakiwa ni 91.


Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bi Salome Abeli, mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo ya meli. Yeye ni mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission akitokea Arusha kwenda Pemba Kikazi leo July 19, 2012.


Mungu Ibariki Tanzania


Imetolewa na:


Katibu Mkuu,
CCM-Texas
Abdallah Nyangassa

No comments:

Post a Comment