SIMBA WAFIKIRIA KUJITOA KAGAME
Yondan anasaini Yanga na mpunga mezani huo |
Simba SC wapo kwenye kikao kujadili juu ya uamuzi wa kushiriki au kutoshiriki
mchuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame,
iliyoanza leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kisa nini? Hawana imani na wenyeji wa michuano hiyo, Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) pamoja na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA). Kivipi? Ni kutokana na kitendo cha vyombo hivyo kumpa
leseni beki wao Kelvin Patrick Yondan achezee Yanga SC, ambao ni wapinzani
wao wa jadi.
Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Simba SC, zimesema
kwamba kitendo cha Yanga kumchezesha Yondan kwenye klabu hiyo leo, katika
mchezo dhidi ya Atletico ya Burundi, kimeikera sana Simba na kinahisi kuna
hujuma wanafanyiwa na TFF na CECAFA.
Ikumbukwe Yondan aliyejiunga na Simba 2006, alijiunga na Yanga mwezi
uliopita ingawa klabu yake inaendelea kudai, ina mkataba naye.
BIN ZUBEIRY ilifanikiwa kuwa chombo cha kwanza cha habari duniani
kuonyesha mikataba yote ya Simba na Yanga dhidi ya Yondan.
Lakini Yondan beki wa kati hodari nchini, mwenyewe hajawahi hata siku
moja kuukana mkataba wowote kati ya hiyo, zaidi ya kusema kujiunga kwake
na Yanga, Simba watajijua wenyewe.
Mwishoni mwa mwaka jana, Yondan alisusa kuchezea Simba na kuamua
kubaki kwao mjini Mwanza, baada ya mechi dhidi Toto African ya mini humo
ya Ligi Kuu.
Na ndipo hapo zilipoanza kuibuka habari za mchezaji huyo kuhamia kwa watani
wa jadi, hadi Mei mwaka huu alipomwaga wino Jangwani. Ingawa Yondan kwa
sasa yupo kwenye kambi ya timu mpya ya Yanga, lakini klabu yake Simba SC
imeendelea kusiistiza huyo ni mchezaji wao halali na sasa inafikiria kujitoa
kwenye Kagame baada ya Vidic wa Tanzania kuchezea Yanga kwenye
michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment