SOCCER: Wichita FC vs Houston FC in Wichita!!!!! |
Ile Timu yenu ya mahiri ya soka, Wichita FC iliyokuwa imeweka kambi kabambe nje kidogo
ya mji, inafuraha kuwatangazia kwamba imerudi mafichoni na inakukaribisha kushuhudia
kabumbu la hali ya juu wakati watakapowakaribisha mahasimu wao wa jadi kutoka Houston
TXJumamosi July 14 kwenye uwanja wa Stryker Soccer Complex (Greenwich & 29 Address:
za Wichita(6:30pm CT)
Meneja wa Timu Mazaza Wa Mtawali (aka B.I.G) anaripoti vijana wake wapo fiti, wenye afya
njema na nidhamu ya hali ya juu. Mazaza anasema anawakati mgumu sana mwaka huu wa
kupanga kikosi kitakachovalia uzi wa kuichambua Houston kutokana na uchu walioonyesha
vijana wakati wa maandalizi ya mechi hii. Kapteni wa Wichita FC Diwani Cheche ameahidi
ushindi mnono na kuundeleza uteja wa Houston FC mbele ya vijana wa Wichita.
TaWichita inawakaribisha kwa moyo mkunjufu wa "Mgeni Njoo..." ndugu zetu wa Houston FC,
na wapemichezo wote wa Wichita na vitongoji vyake kwenye "shughuli" hii kati ya mwezi huu.
Tunauhakika Wichita FC litaibuka kidedea, kama kawa!
|
No comments:
Post a Comment