Sunday, July 1, 2012


YANGA YAICHAPA 2-1 EXPRESSMechi kati ya Yanga na Express ya Uganda, imemalizika wenyeji wameshinda 2-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao yote yakitiwa kimiani na Jerry Tegete dakika ya nne na 20, wakati la mabingwa wa Uganda, beki Ladislaus Mbogo alijifunga katika harakati za kuokoa mpira wa Kiiza Ayoub dakika ya 77. Kipindi cha kwanza Yanga ilitawala mchezo kwa asilimia 60, Express walipiga krosi mbili na shuti moja ambalo halikulenga lango, lakini kipindi cha pili Express walitawala na dakika 20 za mwisho Yanga walikuwa wanaomba mpira usihe. 
Kikosi kilichoanza Yanga, kutoka kulia waliosimama Ally Mustafa 'Barthez', Athumani Iddi 'Chuji', Said Bahanuzi, Oscar Joshua, Jerry Tegete na Nizar Khalfan. Walioinama kutoka kulia ni Kelvin Yondan, Nadir Cannavaro, Juma Abdul, Frank Damayo na Simon Msuva. 

Benchi

Nizar akimpongeza Tegete baada ya kufunga la pili

Vijana wanaingia uwanjani

Wenye timu yao

No comments:

Post a Comment