Tuesday, November 27, 2012

MACHO YOTE KWA JOHN BOCCO ADEBAYOR WA CHAMAZI LEO


John Bocco 'Adebayor'


Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
MSHAMBULIAJI tegemeo wa Tanzania, John Bocco ‘Adebayor’ bado anaongoza kwa mabao katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki, CECAFA Tusker Challenge baada ya mechi 14 kuchezwa hadi hadi jana.
Jumla ya mabao 15 hadi sasa yamefungwa katika mechi 14 za makundi yote matatu, zilizopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Bocco anachuana kwa ufungaji na washambuliaji wa Burundi, Chris Nduwarugira na Suleiman Ndikumana, ambao kila mmoja ana mabao mawili pia.
Wengine ambao hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Yussuf Ndikumana wa Burundi, Mohamed Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito wa Uganda, Yonatal Kebede Teklemariam, Haruna NiyonzimUganda, David Ochieng, Clifton Miheso na Jean Mugiraneza.
Bocco ana nafasi zaidi ya kuongeza mabao katika mechi za kundi hilo, haswa kwenye mchezo dhidi ya Somalia Desemba 1, kwani hiyo ndio timu dhaifu zaidi kwenye Kundi B.
Lakini Bocco kama atacheza kwa kiwango cha mechi dhidi ya Sudan, anaweza akawa mwiba hata leo mbele ya Burundi.
Kwa sasa Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye kikosi cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC) kuzuiliwa na klabu yao.


WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
John Bocco Tanzania 2
Yussuf Ndikumana Burundi 2
Suleiman Ndikumana Burundi 2
Yussuf Ndikumana Burundi 1
Mohamed Jabril Somalia 1(penalti).
Geoffrey Kizito Uganda 1
Brian Umony Uganda 1
Yonatal Teklemariam Ethiopia 1
Haruna Niyonzima Rwanda 1
Jean Mugiraneza Rwanda 1
David Ochieng Kenya 1
Clifton Miheso Kenya 1

No comments:

Post a Comment