|
||
|
MABAO
mawili ya kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ usiku huu
yameipa Zanzibar ushindi wa 2-1 dhidi ya Rwanda, katika mchezo wa
Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker
Challenge uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Kwa
ushindi huo, Zanzibar Heroes imefufua matumaini ya kwenda Robo
Fainali ya michuano hii, ikipanda kileleni mwa Kundi hilo, kwa
pointi zake nne, Rwanda ikishuka nafasi ya pili kwa pointi zake
tatu, sawa na Malawi, wakati Eritrea inashika mkia kwa pointi yake
moja.
Vialli
alifunga mabao yake moja kila kipindi, la kwanza dakika ya sita na
la pili dakika ya 61, yote akionyesha yeye ni fundi na mwenye akili
na maarifa ya soka kutokana na kutulia na kumtungua kipa hodari
kabisa katika ukanda huu, Jean Claude Ndoli.
Rwanda
ilipata bao lake kupitia kwa Dadi Birori dakika ya 79, ambaye
aliingia uwanjani dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Tumaine
Ntamuhanga.
Mchezo
wa leo kama ulivyokuwa mchezo wa kwanza kati ya Malawi na Eritrea
ulitibuliwa na mvua iliyoharibu mandhari ya Uwanja wa Mandela, hivyo
haikuwa wa ufundi zaidi ya ‘butua butua’.
Nahodha
wa Zanzibar, Nadir Heroub ‘Cannavaro’ alisema baada ya mechi
hiyo kwamba wamefuta makosa yao ya mchezo wa kwanza na sasa
Wazanzibari wasubiri Kombe, wakati Haruna Niyonzima wa Rwanda,
alilalamikia Uwanja mbovu leo kuwasababisha kucheza ovyo.
Katika
mchezo wa leo, kikosi cha Zanzibar kilikuwa; Mwadini Ally, Nassor
Masoud ‘Cholo’, Samir Hajji Nuhu, Aggrey Morris, Nadir Haroub
Ali 'Canavaro, Sabri Ali, Khamis Mcha 'Vialli', Abdulaghan Gulam,
Jaku Juma, Seif Abdallah/Adeyom Saleh Ahmed dk88 na Suleiman Kassim
‘Selembe’.
Rwanda;
Jean Claude Ndoli, Emery Bayisenge, Hamdani Bariyanga, Ismail
Nshutiyamagara, Mwemere Ngirishuti/Jean Claude Iranzi dk46, Jean
Baptiste Mugiraneza, Haruna Niyonzima, Jimmy Mbagara, Jerome Sina,
Jean D’Amour Uwimana/Fabrice Twagizimana dk24 na Tumaine
Ntamuhanga/Dadi Birori dk66.
MSIMAMO
KUNDI C:
P
W D L GF GA GD Pts
Zanzibar
2 1
1 0 2 1
1 4
Rwanda 2 1 0 1
3 2 1 3
Malawi
2 1
0 1 3 4
-1 3
Eritrea
2 0 1 1 2
3 -1 1
|
||
|
||
|
||
|
Vialli
kushoto akishangilia bao lake la pili, kulia ni Suleiman Kassim
'Selembe'
|
Wachezaji
wa Zanzibar wakishangilia bao la pili kwa staili ya kupiga kasia
|
No comments:
Post a Comment