MH. Balozi Tuvako Manongi na MH. Naibu mwakilishi wakiwa kwenye kikao na viongozi wa Tanzania NY Community, Katika kikao hicho cha utambulisho kwa viongozi hao kwa balozi na kumfahamisha rasmi jukumu la kuwa mlezi wa viongozi na jumuiya. Mh. Balozi alikubari wazifa huo kwa moyo mweupe na kuhaidi kushirikiana bega kwa bega na viongozi hao kwa kadri ya uwezo wake wote akishirikiana na Mh. Naibu mwakilishi Ramadhan Muombwa Mwinyi. Nakatika kikao hicho Mh. Balozi Manongi alikabizi kwa mwenyekiti wa jumuiya bwana Hajji Khamis mwongozo kuhusu utaratibu wa watanzania wanaoishi ughaibuni kushiriki kutoa maoni yao kuhusu upatikanaji wa katiba mpya.
Hapa Mh. Naibu Mwakilishi Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akifafanua jambo mbele ya viongozi wa jumuiya katika kikao hicho, Mh. Muombwa alipata pia fursa ya kukutana na viongozi wa Tanzania NY Community kwa mala ya kwanza. Viongozi wa jumuiya walimkaribisha NY na atakuwa bega kwa bega na viongozi hao kadri ya uwezo wake kama ilivyo kwa Mh. Balozi Manongi kuakikisha kila kitu kilichozungumzwa hapa kina enda sawa kama kilivyo pangwa kwa manufaha ya community.
Kikao kikiendelea kuna mweka azina wa community bwana Temba, katibu wa community bwana Shaban Mseba, mwenyekiti wa community bwana Hajji Khamis na dada Lydia Jengo-Waluye kama mjumbe mwenye mtazamo wa kimaendeleo.
MH. Balozi Manongo akimkabizi mwenyekiti wa jumuiya bwana Hajji Khamis mwongozo kuhusu utaratibu wa watanzania wanaoishi ughaibuni kushiriki kutoa maoni yao kuhusu upatikanaji wa katiba mpya
Kutoka kushoto ni mweka azina wa community na CEO wa Temba Engineering, akifuatiwa na Mh. Balozi Manongi akikabizi mwongozo huo kwa bwana Hajji Mwenyekiti wa Jumuiya na mwisho ni Mh. Naibu mwakilishi balozi Muombwa wakishuudia makabiziano hayo yaliyo fanyika katika office za Ubalozi New York City.
Picha ya pamoja baada ya kikao hicho kumalizika ofisini hapo, kama kumbukumbu
Katibu wa jumuiya bwana Mseba akipata Ukodak na Mh. Naibu Mwakilishi balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi baada ya kikao
CEO Temba Engineering na mweka azina wa community akipata Ukodaki na Mh. Naibu Mwakilishi balozi Ramadhan Muombwa baada ya kikao.
Bwana Shaban katibu wa community akipata Ukodak na Mh. Balozi Manongi |
Ny Ebra nae akipata Ukodak na waheshimiwa kwa heshima na tahazima |
No comments:
Post a Comment