Sunday, December 16, 2012

‘Hausigeli’ amnywesha mkojo bosi wake, ahukumiwa jela


HARARE, Zimbabwe

MFANYAKAZI za ndani ‘hausigeli’ amehukumiwa kifungo cha miezi miwili jela na viboko, kwa kosa la kumnywesha mkojo bosi wake kutokana na hasira ya kutolipwa mshahara wake kwa wakati.
Rita Chakwesha mwenye umri wa miaka 25, ambaye aliajiriwa katika nyumba iliyopo kwenye Barabara ya Avenue mjini Harare, kwa makusudi alimnywesha mwajiri wake Sharlotte Chivavarirwa maji yaliyokuwa na mkojo ndani yake.
Chakwesha alionekana mbele ya Hakimu Barbra Masinire huko Harare, akihukumiwa kwa makosa hayo, huku akijitetea kuwa alikuwa akifanya hivyo kutokana na kutopewa ujira wake kwa miezi miwili.
Mshauri wa Jimbo la Francesca Mukumbiri aliiambia mahakama kuwa Novemba 5 majira ya saa 11 jioni, Chivavarirwa alirejea nyumbani akitokea kazini, na mara baada ya kufika alimwomba msichana wake wa kazi Chakwesha ampe maji kutoka katika jokofu.
Chakwesha alienda na kumiminia maji ambayo tayari alikuwa ameyatia mkojo na kumpa bosi wake kwamba ayafurahie kwani ni maji yaliyokuwa na ladha nzuri.
Mama huyo mwenye nyumba baada ya kufungua jokofu aliona glasi yenye kitu chenye rangi ya manjano na harufu mbaya, hivyo akahisi kuwa huenda ni mkojo.
Hata hivyo, Chakwesha hakuishia hapo, alijikuta akitoa siri kwa rafiki wa karibu na Chivavarirwa, ambaye hakutaka kuitunza siri ile.
Rafiki huyo alikwenda kumweleza hali halisi Chivavarirwa ambaye aliamua kulipeleka suala hilo chini ya sheria na hivyo Chakwesha alikamatwa.
Kabla ya kuburutwa mahakamani, Chakwesha alikiri kutenda kitendo hicho cha ajabu na kwamba hali hiyo ilitokana na mwajiri wake kutomlipa ujira wake “Ndanga ndabatwa nemweya wehutsinye,” Chakwesha aliiambia mahakama

No comments:

Post a Comment