Tuesday, December 4, 2012

Uhuru Seleman azungumzia Maisha yake Simba SC


Uhuru Selemani
Kama wewe ni shabiki wa soka la bongo na umekua ukilifatilia, hii ni nafasi yako kusikia aliyoyasema mchezaji Uhuru Selemani aliyehamia Azam Fc akitokea Simba Sc.

Kwenye exclusive interview na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM, Amesema kwenye maisha yake ya soka kuna mambo mawili tu ambayo yamewahi kumuumiza sana, moja ni kifo cha Patrick Mafisango aliekua akicheza nae Simba na jingine ni kuwekwa benchi kwa msimu mzima Simba.
Hii ni moja ya picha zake za mwanzo wakati ameanza mazoezi na Azam

Kuhusu sababu za yeye kuwekwa benchi kwa msimu mzima namkariri akisema “sitaki kuficha, mi naamini kuna kiongozi mmoja ndani ya Simba ambae alikua hataki mafanikio yang lakini sielewi kwa nini namjua kabisa ila siwezi kutaja jina lake”

“Nafikiri huyo mtu alikua karibu sana na mwalimu na alikua na nafasi ya kuongea sana na mwalimu kwa hiyo ndio alikua anapanga mimi nisitumike kwenye timu, sijui ni kwa sababu gani na sijawahi kukorofishana nae” – Uhuru


Kwenye sentensi nyingine Uhuru amesema kuhusu kukaa kwake benchi aliwahi kumuuliza mwalimu lakini hakumjibu chochote zaidi ya kumwambia kwamba yeye ni mchezaji bora anatakiwa kuendelea kufanya mazoezi manake ni mchezaji mzuri ambae anaweza kufanya kitu chochote.

Namkariri tena akisema “mwalimu alikua halioni hilo, viongozi wa juu wa timu waliliona pia lakini walinyamaza kama rais wa timu ananijua nina mchango gani kwenye timu lakini hakuwahi kuuliza hata siku moja kwa nini Uhuru hachezi”

Kwa kumalizia Uhuru amesema “Kukaa benchi bila kupewa jezi imeniuma sana, nataka watu wajue hiyo imeniuma sana na sikutegemea kama Simba wanaweza kunifanyia kitu kama hicho kwa sababu nimeifanyia Simba mambo makubwa sana, nimeingia Simba nimeipa taji la ubingwa mara mbili, makombe mbalimbali na ngao za hisani.. ni kwa muda mfupi ambao nimekuwepo Simba japokua kuna watu ambao nashirikiana nao lakini kwa upande wangu naamini nimetoa mchango mkubwa”

No comments:

Post a Comment