Tuesday, December 4, 2012

Tusker Challenge Cup'12 : Kenya Vs Zanzibar , Uganda vs Kili ( Semi-Final )

Katika Robo Fainali ya kwanza Kenya imeifunga Malawi 1-0 kwa bao la Mike Barasa dakika ya 56 na sasa itamenyana na Zanzibar katika Nusu Fainali keshokutwa.

Wachezaji wa Kenya
Nayo Uganda ikaibanjua Ethiopia kwa mabao 2-0. Mabao ya Geoffrey Kizito na Robert Ssentongo dk.60 katika Robo Fainali ya pili iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala yalitosha kuwapeleka Nusu Fainali ambako watakutana na Tanzania Bara katika Alhamisi usiku

Waganda wakishangilia bao la Kizito

No comments:

Post a Comment