Saturday, December 22, 2012

TAIFA STARS YAIFUNGA CHIPOLOPOLO 1-0 UWANJA WA TAIFAMchezaji wa timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo James Chamanga akiruka juu kuwania mpira huku mchezaji wa timu ya Tanzania Taifa Stars Mrisho Ngasa akiuvizia, katika mchezo wa FIFA wa kirafiki unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Timu ya Tanzania Taifa Stars imeifunga Chipolopolo ya Zambia goli 1-0 na kutoka kifua mbelea uwanjani , mfungaji wa goli hilo akiwa Mrisho Ngasa katika dakika ya 45 ya mchezo huo.

Mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa akishangilia na kupongezwa na wenzake mara baada ya kufunga goli la mkwanza katika mchezo huo.
Wachezaji wa Taifa Stars wakitoka nje ya uwanja kwa mapumziko baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwenye uwanja wa Taifa.
Mashabiki wa timu ya Taifa Stars wakishagilia mara baada ya Mrisho Ngasa kufungo goli la kwanza dhidi ya Chipolopolo katika mchezo huo
Kikosi cha timu ya Zambia kikiwa katika picha ya pamoja
Mnazi Mkubwa wa Timu ya Yanga na Taifa Stars Heavy D. akinyanyua skafu yake yenye bendera na maneno ya Tanzania wakati wimbo wa taifa ukiimbwa kabla ya mchezo huo.

Kulia ni Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini Zambia Kalusha Bwalya na mabalozi wa Zambia nchini Judith Kangoma-Kapijimpanga na Balozi Tanzania nchini Zambia Bi. Grace Mujumi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya taifa ya Zambia wakishangilia timu yao katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment