Sunday, December 23, 2012

TZHOUSTON Community : Vijana wawachapa kwa taabu Wazee pungufu 2-1

Timu ya Under 34's hapo jana iliwafunga wazee wa Houston kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali na wa kusisimua.Vijana wakiongozwa na Kocha-mchezaji Himidy Mshale, Sekulu, Andrew Sanga, God Mahinya, Hamis Muller na beki lililocheza kiundavaundava siku ya jana Raheem Chomba walifanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza kwa shuti la umbali wa mita kama 40 hivi lililopigwa na Himidy . 

Wazee wakijadiliana wakati wa mapumziko
 Wazee walikuja juu na kusawazisha bao hilo katoka dakika ya 40 kupitia kwa Bitebo baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la Vijana.Hadi mapumziko matokeo yalikuwa 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kunako dakika ya 60 refa kutoka Mexico Pablo Suarez alimtoa kwa kadi nyekundu Bitebo baada ya yeye(Bitebo) kupigwa buti na Raheem.

Mshauri wa Vijana Abou Barnes akiwapa mkakati wakati wa mapumziko
Kadi hiyo haikuwakatisha tamaa wazee ambao waliendelea kuumiliki mpira  muda mwingi wa mchezo.Dakika ya 70 wachezaji Charles Mbassa na Sekulu waligongana katikati ya uwanja na wote kwenda chini na kwa mshangao wa wengi refarii akatoa kadi nyingine nyekundu kwa mchezaji wa wazee Charles. 
Wazee wakijadiliana wakati wa mapumziko
 Baada ya hapo vijana walitawala mpira kwa kipindi kirefu . wakati kila mtu akijua matokeo yatakuwa sare Ally Mtumwa aliwapatia bao la pili Vijana katika dakika ya 88 na kuamsha shangwe za vijana waliokuwepo uwanjani. Bao hilo lilikuwa la kukata uteja wa miaka 3 ambapo wazee wamekuwa wakiwafunga vijana kila wakikutana. Baada ya mechi hiyo watu waliendelea kuburudika na vinywa na nyama choma zilizokuwa zimeandaliwa na wana D-Squad
Michezo Furaha : Sekulu (kushoto) na Justice Jaden baada ya mechi

Faza G na Hamees Muller

Refarii Pablo akiwa na wazee aliowalima red card , Charles (mwenye hasira kushoto) na Bitebo

No comments:

Post a Comment