Na Mahmoud Zubeiry
Straika wa
kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi wa Simba ameuzwa kwa klabu ya Etoile
du Sahel ya Ligi Kuu ya Tunisia kwa dola za Kimarekani 300,000 (Sh.
milioni 472)
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC,
Zacharia Hans Poppe, ameiambia bongostaz.blogspot.com kuwa, Okwi
amekamilisha vipimo na kila kitu na tayari amesaini mkataba.
“Tunasubiri kulipwa fedha zetu tu, viongozi watakwenda Tunisia kuchukua fedha za mauzo ya mchezaji huyo,”alisema Poppe.
Okwi amekuwa akipiga chenga kuripoti kambini Simba SC na alikuwa hata hapokei simu za viongozi wa klabu hiyo kila alipopigiwa.
Kufuatia hatua hiyo, uongozi ulimuengua kwenye programu ya safari ya Oman na sasa inabainika ametua Sahel.
Okwi,
aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 aliisajiliwa Simba akitoea SC Villa
ya Uganda mwaka 2010 akiwa yosso wa miaka 17, akisajiliwa kwa dau la
dola za Kimarekani 40,000 (Sh. milioni 63).
Baada ya kumaliza
mkataba wake wa awali, Desemba mwaka jana aliongeza mkataba wa miaka
miwili na Simba ambao kabla hajaanza kuutumikia, ameamua kuhamia Sahel.
No comments:
Post a Comment