Monday, January 14, 2013

Meneja Machinga Complex Dar avunjwa mkono

MGOGORO wa vizimba katika soko la wafanyabiashara wadogo la Machinga Complex lililoko jijini Dar es Salaam umeingia hatua nyingine baada ya Meneja wa soko hilo, Nyamsukura Masondore kuvamiwa na wafanyabishara hao, kumpiga hadi kumvunja mkono.

Machinga Complex
Tukio hilo lilitokea Januari 7, mwaka huu, wakati Meneja huyo akiwa ziarani kuhakiki umiliki halisi wa mpangaji na ulipaji wa kodi kwa vizimba hivyo. Akiwa katika mahojiano na Mwananchi, Msondore alisema kuwa wakati wa zoezi hilo la kuhakiki wapangaji na walipakodi ghafla alivamiwa na watu wasiopungua wanane na kumpiga hadi kumvunja mkono.
“Nilikuwa nimeongozana na viongozi wenzangu kwenye shughuli hiyo ya uhakiki, ghafla nikavamiwa na watu ambao wanadaiwa ni wafanyabiashara wa hapa kwenye jengo na wengine wa Soko la Karume wakanipiga hadi kunivunja mkono,” alisema Masondore.

Masondore alisema kuwa alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Pangani katika Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam na kupewa RB ya polisi no Ila/rb/75/2013 kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili, na uchunguzi wa polisi unaendelea.
Aliongeza kuwa kutokana na tukio hilo alishindwa kuendelea na uhakiki huo wa vizimba na walipakodi na kuelekea Hospitali ya Amana iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo ndipo anapata matibabu hadi sasa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi Komba alisema kuwa hana taarifa za kutokea kwa vurugu hizo katika jengo hilo la wafanyabiashara wadogo.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa jengo hilo, Abubakari Rakesh ameulalamikia uongozi wa jengo kuwa tangu kuzinduliwa kwa gulio lililopo ndani ya jengo hakuna ufuatiliaji wowote uliofanyika ili kuutaka kujua maendeleo ya wafanyabiashara.
Alisema kuwa uzinduzi huo ambao ulifanywa na Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Abdalah Chaurembo haukuwa wazi kwa kila mtu jambo ambalo halikupangwa kufanyika hivyo tangu taratibu hizo za uzinduzi zianze.
“ Uzinduzi huu ulikuwa wa kimyakimya jambo ambalo hatukupanga hivyo, tulitegemea matangazo mbalimbali yawekwe kwa ajili ya kuwakumbusha wafanyabiashara na wananchi pia juu ya uzinduzi, lakini haukufanyika hivyo, naweza kusema ulikuwa uzinduzi wa funika kombe mwanaharamu apite”, alisema Rakeshi.
Rakesh aliongeza kuwa uongozi wa jengo hilo ulitakiwa uwe mstari wa mbele kwa ajili ya kutetea maslahi ya wafanyabiashara wanaofanya biashara zao hapo lakini badala yake uongozi huo haupo bega

No comments:

Post a Comment