Tuesday, February 19, 2013

Bayern 3-1 Arsenal : mwaka wa 8 bila kombe


Toni Kroos akishangilia goli la kwanza la Bayern
Vigogo wa Ujerumani, Bayern Munich usiku wa kuamkia leo Jumatano wamezidi kumuweka matatizoni zaidi Kocha Arsene Wenger kwa mashabiki wa Arsenal baada ya kuichapa timu yake mabao 3-1.

Arsenal iliyokuwa nyumbani Emirates London, ilikutana na kipigo hicho hali inayozidi kuamsha mgogoro kati ya Wenger na mashabiki ambao walionyesha kupoteza imani na kikosi chao hata kabla ya mechi hiyo.
Ligi ya Mabingwa ndiyo michuano pekee ambayo Arsenal wanapambana kupata kombe baada ya kuwa wameng’olewa katika Kombe la FA baada ya kupata kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Blackburn Rovers.

2-0 : Dakika ya 21 Thomas Mueller anatupia la pili 
Kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Wajerumani hao, ni sawa na kuthibitisha kwamba Arsenal haitabeba kombe lolote katika kipindi cha miaka nane. Labda itokee miujiza mjini Munich na wao wasonge mbele hadi katika robo fainali.
Katika mechi ya jana, Bayern pamoja na kuwa wenyeji walicheza kwa kujiamini zaidi na kufanikiwa kupata mabao yao mawili katika kipindi cha kwanza kupitia Toni Kroos aliyepiga shuti katika ya mabeki wa Arsenal katika dakika ya 7 na Thomas Muller aliyepiga la pili dakika ya 21.

Wenger na msaidizi wake Steve Bould hawajui kinachoendelea
Mjerumani Lukas Podolski aliifungia Arsenal bao pekee kwa kichwa katika dakika ya 55. Wakati Arsenal wanaonekana kupania kusawazisha, Mario Mandzukic akawazika kwa bao la tatu katika dakika ya 77.

Mechi nyingine ya raundi ya 16 Bora jana ilikuwa ni kati ya FC Porto ikiwa nyumbani iliizamisha Malaga ya Hispania kwa bao 1-0 lililofungwa na Moutinho.

No comments:

Post a Comment