Monday, February 25, 2013

Mkutano wa Jumuiya ya Watanzania - New York wafana

Mhe. Naibu Mwakilishi Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa mataifa New York, Ramadhani Muombwa Mwinyi (kulia)akiufungua mkutano mkuu wa kwanza wa Jumuiya ya Watanzania New York, uliofanyika Jumapili Feb 24, 2013 Harlem, New York nchini Marekani na kuhudhuriwa na Wanajumuiya hiyo. Watu wengine katika picha tokea shoto ni Omar Ally wa Pennsylvania ambae ni mwenyekiti wa Zanzibar DIASPORA, Shabani Mseba, katibu Jumuiya ya Watanzania New York na Hajji Khamis, Mwenyekiti Jumuiya ya Watanzania New York .

 Kutoka kushoto ni Shabani Mseba, Hajji Khamis, Mhe Ramadhani Muombwa Mwinyi na Mama Kiswaga
Mshauri wa masuala ya Uhamiaji Bw. Orlando akielezea masuala hayo
Muasisi wa chama cha siasa CUF,  Dr. Chemponda akiwapongeza wanajumuiya wa New York kwa kuweka itikadi za vyama pembeni na kuwa wamoja kama Watanzania na si CCM, CHADEMA, CUF au chama chochote cha siasa wanachoshabikia.

Wageni waalikwa wakiwemo maafisa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York

Juu na chini ni Wanajumuiya wa New York wakifuatilia mkutanoNo comments:

Post a Comment